Monday, October 28, 2019

Marubani wa Southwest Airlines: Walikuwa wakichukua filamu za moja kwa moja kutoka katika choo cha ndege hiyo


Rubani aliambia mfanyakazi wa ndege kwamba kamera hizo zilikuwa siri kubwa na mkakati wa kiusalamaHaki miliki ya picha
Image captio
Mfanyakazi wa kampuni ya ndege ya Southwest Airlines amewasilisha kesi mahakamani akiwashutumu marubani wawili kwa kuficha kamera katika choo cha ndege hiyo na kuwachukua picha za moja kwa moja abiria ambao walikuwa wakienda kujisaidia.
Renee Steinaker anadai kwamba aliwapata marubani hao wakati wa safari ya ndege ya mwaka 2017 kutoka Pittsburgh hadi Phoenix.
Rubani Terry Graham alimtaka kukaa katika chumba cha rubani na rubani mwenza Ryan Rusell, wakati alipotumia choo hicho, mashtaka hayo yanasema.
Rubani na kampuni ya ndege ya South West Arlines wamekana kwamba kulikuwa na kamera iliyokuwa ikiwachukua abiria na wafanyakazi waliokwenda msalani.
Kampuni hiyo imesema kwamba kisa hicho kilikuwa cha kushangaza.
Bi Steinaker anadai kwamba bwana Russell alimuonya kutosema kitu kuhusu kamera hiyo ambayo alisema ilikuwa mkakati wa usalama.
Mfanyakazi huyo aliripoti kisa hicho kwa kampuni hiyo, lakini anadai msimamizi mmoja alimuagiza kutomwambia mtu yeyote kilichotokea.
Marubani hao hawakuitwa na kampuni hiyo ya ndege na wanaendelea na kazi yao kawaida kulingana na mashtaka hayo.
''Madai yaliowasilishwa ni ya kikatili'', wakili anayemwakilisha bi Steinaker aliiambia BBC.

Je kampuni hiyo na marubani wake wamesema nini?

Katika taarifa kampuni ya ndege ya Southwest Airlines iliambia BBC kwamba kampuni hiyo haiweki kamera katika vyoo vya ndege.
Awali , kampuni hiyo ya ndege ya Marekani ilikataa kutoa tamko kuhusu kesi hiyo .
Lakini katika taarifa nyingine , ilisema imechunguza madai hayo na kupata kwamba hakukuwa hata na kamera moja katika choo.
Southwest itapinga mashtaka hayo , ilisema.
''Wakati kisa hicho kilipotokea siku mbili zilizopita, tulichunguza madai hayo na kuangazia hali hiyo na wafanyakazi waliohusika''.
Kisa hicho kimedaiwa kutokea wakati wa safari ya 2017 kutoka Pittsburgh hadi Phoenix
Kisa hicho kimedaiwa kutokea wakati wa safari ya 2017 kutoka Pittsburgh hadi PhoenixHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKisa hicho kimedaiwa kutokea wakati wa safari ya 2017 kutoka Pittsburgh hadi Phoenix
"Tunaweza kuthibitisha kutoka kwa uchunguzi wetu kwamba hakukuwa na kamera chooni, kisa hicho hakifai na kwamba kampuni hiyo haiwezi kukikubali''.
BBC imeomba tamko kutoka kwa mawakili wanowawakilisha marubani hao.
Katika majibu yao yalioandikwa kwa walalamishi bwana Russell na bi Graham walikiri kwamba kulikuwa na kipakatalishi katika chumba hicho cha marubani lakini walikana madai mengine yoyote, CNN iliripoti.

Je mashtaka hayo yanasemaje?

Saa mbili kabla ya safari ya ndege kuanza mnamo tarehe 27 Februari 2017, bi Graham alimuomba bi Stainaker kusalia katika chumba hicho cha marubani huku yeye akienda chooni , yalisema malalamishi hayo.
Kulingana na sera ya kampuni hiyo ya ndege wafanyakazi wawili wanafaa kuwepo katika chumba hicho cha ndege kila mara.
Bwana Russell alikiri kwamba kamera ilikuwa ikichukua watu moja kwa moja , huku akiwa na wasiwasi katika uso wake, kabla ya kumshauri bi Stainaker kutoambia mtu yeyote na kwamba ulikuwa mkakati wa kiusalama, yamesema malalamishi.
Kamera hizo zilikuwa na siri kubwa zikiwa zimewekwa katika kila ndege aina ya 737-800 , ilidaiwa kwamba bwana Graham alimwambia mfanyakazi mmoja wa ndege.
Na kufuatia maelezo ya bwana Russell, bi Stainaker alipiga picha ya kipakatalishi hicho na simu yake, yalisema mashtaka hayo.
Wakati bi Stainaker alipolalama, msimamizi mmoja alimwambia kunyamaza kuhusu suala hilo , na kwamba iwapo itajulikana hakuna mtu atakayesafiri kwa kutumia kampuni hiyo ya ndege.
Presentational grey line
Mashtaka hayo ya Bi Steinaker yanataka alipwe $50,000 kama fidia kutoka kwa kampuni ya Southwest Airlines pamoja na marubani.
Bwana Goldman alisema mteja wake alikua amedhurika na suala hiyo ambalo lilimsababishia dhiki kali.
Mashtaka hayo yaliwasilishwa katika kaunti ya Maricopa , jimbo la Arizona, lakini imehamishwa katika mahakama ya wilaya mjini Arizona.
Hakuna tarehe ya kusikilizwa kwa keshi hiyo imewekwa kufikia sasa.

Abu Bakr al-Baghdadi: Tunachokijua kuhusu uvamizi wa Marekani na mauaji yake Syria


Rais Trump akivihutubia vyombo vya habari kufutia kifo cha Baghdadi
Rais Donald Trump ametangaza kwamba kiongozi aliyekuwa akijificha wa kundi la Islamic State , Abu Bakr al Baghdad alijiuwa mwenyewe wakati wa uvamizi wa kikosi maalum cha Marekani nchini Syria.
Hiki ndicho tunachojua kuhusu operesheni hiyo.

Ni wapi na lini ilitekelezwa?

Katika tangazo la runinga , bwana Trump alitangaza kwamba gaidi huyo nambari moja duniani amefariki wakati wa uvamizi hatari wa usiku kaskazini magharibi mwa Syria na vikosi maalum vya Marekani.
Marekani ilikuwa imetoa kitita cha dola milioni 25 kwa habari kuhusu alipo Abu bakr al BaghdadiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMarekani ilikuwa imetoa kitita cha dola milioni 25 kwa habari kuhusu alipo Abu bakr al Baghdadi
Rais alisema kwamba ndege aina ya helikopta iliokisafirisha kikosi hicho maalum iliondoka kutoka eneo ambalo halikutajwa baada mwendo wa saa kumi na moja saa za Marekani siku ya Jumamosi, wakati yeye na viongozi wengine walikusanyika katika chumba cha Ikulu ya Whitehouse.
Ndege zilisafiri kwa muda wa saa moja na dakika 10 kutoka maeneo tofauti, hiuku opetresheni ya ardhini ikifanyika kwa muda wa saa mbili, aliongezea.
Maafisa waliambia vyombo vya habari nchini Marekani kwamba mapema siku ya Jumapili nchini Syria, vikosi maalum vya Marekani vililenga eneo moja la kijiji cha Barisha mkoani Idlib takriban kilomita 5 kusini mwa mpaka wa Uturuki.
Eneo alilokuwa kiongozi huyo wa Islamic State Syria
Presentational white space
Idlib ndio ngome ya mwisho ya upinzani dhidi ya serikali ya Bashar al Asad.
Inatawaliwa na muungano wa wapiganaji wa Jihad ambao unakinzana na Kundi la Islamic State , lakini mamia ya wapiganaji wa IS wanaaminika kupiga kambi katika eneo hilo.
Jeshi la Syria linaloungwa mkono na Syria lipo mashariki, magharibi na kusini.

Jinsi uvamizi huo ulivyofanyika

Bwana Trump alisema kwamba vitengo vya ujasusi nchini Marekani vilimchunguza Baghdad kwa wiki kadhaa kabla ya operesheni na kwamba walijua eneo hilo lilikuwa na mahandaki kadhaa, huku mengi yakiwa na mwisho wake.
Siku ya Jumamosi , rais aliamrisha ujumbe uliohusisha kundi moja la wanajeshi maalum , ndege nane na meli nyingine nyingi.
Picha zikimuonyesha rais donld Trump na viongozi wengine wa kisiasa na kijeshi wakiwa katika chumba kimoja cha Ikulu ya Whitehouse
Ndege hizo zilipaa juu ya anga ya Uturuki, mbali na maeneo yanayodhibitiwa na majeshi ya Syria pamoja na yale ya Urusi.
Urusi ilishirikiana na kufungua nga yake kwa operesheni hiyo ya Marekani licha ya kutoambiwa kile kilichokuwa kikijiri kulingana na rais Trump.
''Operesheni hiyo ya kuingia na kutoka ilikuwa hatari mno. Kulikuwa na wakati ambapo tungekabiliwa vilivyo'' , alisema .
''Ndege zetu zilipaa chini chini lakini kwa mwendo wa kasi''.
Huku ndege hizo zikikaribia katika nyumba hiyo zilishambuliwa lakini Trump anasema mashambulizi hayo yalimalizwa haraka.
Mkaazi mmoja wa Barisha anasema kwamba ndege hizo za Marekani zilishambulia nyumba mbili na kuiharibu kabisa mojaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMkaazi mmoja wa Barisha anasema kwamba ndege hizo za Marekani zilishambulia nyumba mbili na kuiharibu kabisa moja
Mwanakiji mmoja kutoka eneo la Barisha aliambia BBC kulikuwa na mashambulizi kutoka kwa helikopta hizo kwa zaidi ya dakika 30 kabla ya vikosi vya ardhini kuingia eneo hilo, akiongezea kwamba ndege hizo zilishambulia nyumba mbili na kuiharibu kabisa mojawapo.
Baada ya ndege hizo kutua , wanajeshi hao maalum walilipua mashimo katika kuta ya nyumba hizo ili kukwepa kuingia ndani kupitia mlango wa mbele uliowekwa vilipuzi na baadaye kuanza kuondoa vifusi kulingana na Trump.

Unaweza pia kusoma:

Rais huyo alisema kwamba Baghdad alifariki baada ya kutorokea katika handaki lililo na mwisho, akilia na kupiga kelele.
Hakuna uthibtisho huru wa mauaji ya BaghdadiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionHakuna uthibtisho huru wa mauaji ya Baghdadi
Watoto 11 waliondolewa katika nyumba hiyo bila majeraha kufikia wakati huo, huku watu wakisalimu amri na wengine kupigwa risasi.
''Aliyekuwa amesalia alikuwa Baghdadi pekee katika handaki pamoja na watoto watatu'', aliongezea.
''Alifika mwisho wa handaki , huku mbwa wetu wakimfukuza . Alikuwa ameweka vilipuzi katika nguo yake ya ndani na akajilipua na watoto hao watatu''.
''Mwili wake ulikatwakatwa na mlipuko huo huku handaki hilo likiuangukia'' , aliongezea.
Picha na kanda za video kuhusu kilichotokea baada ya uvamizi huo wa Marekani zilionyesha vifusi vya jengo lililoharibiwa pamoja na gari lililochomeka likiwa na mashimo chungu nzima ya risasi.

Kwa nini Marekani ina hakika Baghdadi amefariki?

Bwana Trump amesema kuwa matokeo ya vipimo vya mabaki ya mtu aliyejilipua katika handaki hilo yalionyesha kwamba alikuwa Baghdadi.
Ilichukua takriban muda wa dakika 15 baada ya kufariki.
''Vipimo hivyo vilifanywa na wataalam waliosafiri na vikosi hivyo maalum na walikuwa na sampuli ya vinasaba vya Baghdadi'', aliongezea.
Wataalam hao pia walibeba vipande vya mabaki ya mwili wake katika ndege hizo, kulingana na Trump. Hakujakuwa na uthibitisho huru kuhusu kifo cha Baghdad. Wafuasi wa IS wamekuwa wakionyana kuhusu kuamini tangazo hilo la Marekani.

Je kuna majeraha mengine?

Rais huyo alisema: hakuna hata mwanajeshi ama afisa mmoja wa Marekani aliyeuawa katika operesheni hoyo, huku idadi kubwa ya wapiganaji wa Baghdadi na washirika wao wakifariki naye.
Chombo cha habari cha Jihadi mjini Idlib lkimesema kwamba basi la raia lilishambuliwaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionChombo cha habari cha Jihadi mjini Idlib lkimesema kwamba basi la raia lilishambuliwa
Wake wawili wa Baghdadi ni miongoni mwa waliokufa
Bwana Trump anasema kwamba wanawake hao walipatikana wakiwa wamevalia fulana za ndani zilizowekwa vilipuzi ambavyo havikulipuliwa.
Mbwa wa Marekani alijeruhiwa katika handaki hilo mahala ambapo Baghdadi alifariki , kulingana na Trump .
Haijajulikani iwapo wafuasi wa IS ama watoto waliokamatwa walijeruhiwa.
Bwana Trump alisema kwamba wapiganaji hao kwa sasa wanazuiliwa huku watoto hao wakiwekwa chini ya usimamizi wa mtu ambaye hakutajwa.

Kwa nini Baghdadi alijificha Idlib?

Mji wa Barisha upo mamia ya kilomita kutoka eneo la jangwa lililo mashambani katika mpaka wa Syria na Iraq ambapo Baghdadi aliaminika kujificha.
Bwana Trump alisema kwamba, Baghdadi alikuwa Idlib kwa kuwa alikuwa na lengo la kujenga upya jeshi lake la wapiganaji wa IS baada ya vikosi vya Kikurdi vinvyoongozwa na Marekani kuteka ngome zake za mwisho zilizosalia karibu na kijiji cha Baghuz kilicho mashariki mwa Syria mwezi Machi.
''Hiyo ndio sababu iliomfanya kusalia katika eneo hilo'', rais huyo aliongezea. Hilo ndio eneo muhimu unapozungumzia kujenga upya kundi hilo.
Anasema kwamba ripoti muhimu za kijasusi kuhusu mipango ya siku zijazo ya Baghdadi ilipatikana wakati wa shambulio hilo na kwamba Marekani itamsaka yeyote yule atakayemrithi.
''Tunawajua watakaomrithi. Na tayari tumeanza kuwaaangazia''.

Je Abu Bakr al-Baghdadi ni nani?

Alizaliwa 1971 katika eneo la Samarra nchini Iraq.
Akiwa angali mtoto alidaiwa kupenda sama kusoma Quran na kufuata sheria za kidini, akiwalaumu ndugu zake wasiofutwa vizuri dini ya Kiislamu.
Lakini ilikuwa wakati ambapo alikuwa anafuzu kupata Stashahada ya somo la Quran katika chuo kikuu cha Saddam Husein , ndio wakati alijihusisha na msimamo mkali wa kundi hilo.
Mwisho wa mwaka 2000 alikuwa ameanzisha kundi linalofuata sunna na aliendelea hadi kushirikishwa na kundi la al-qaeda nchini Iraq ambapo kundi la Islamic state lilibuniwa.
Tangu 2014 amesalia mkimya kwa muda mrefu huku kukiwa na uvumi wa kifo chake ambao haujathibitishwa.

Sunday, October 27, 2019

Stormzy na Meghan Markle ni miongoni mwa watu weusi walioorodheshwa kati ya wale walio na ushawishi mkubwa zaidi Uingereza


Meghan Markle and StormzyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Stormzy, Meghan Markle na Raheem Sterling wametajwa miongonbi mwa watu weusi walio na uwezi mkubwa nchini Uingereza.
Muhariri wa jarida la Vogue Edward Enninful , mwanamitindo Adwoa na Reggie Yates pia wameorodheshwa katika orodha hiyo ya 2020.
Ismail Ahmed ambaye ndiye mkuu wa kampuni ya fedha ya WorldRemit , ndiye anayeongoza katika orodha hiyo.
Orodha hiyo inashirikisha watu 100 wenye mizizi ya Afrika, Afrika na Caribean na Waafrika wa Marekani wanaofikiriwa kuwa na ushawishi mkubwa.
Majina mengine maarufu katika orodha hiyo ni Idris Elba, Anthony Joshua, Dina Asher-Smith na Naomie Harris.
Dina Asher-Smith, Raheem Sterling na Adwoa AboahHaki miliki ya picha
Image captionDina Asher-Smith, Raheem Sterling na Adwoa Aboah wote waliorodheshwa katika orodha hiyo ya 2020
Ismail Ahmed alianzisha kampuni yake 2010 akitumia fidia kutoka kwa Umoja wa mataifa kwa kufichua kashfa kubwa ya iufisadi.
Kampuni yake inalengwa kuwasaidia wahamiaji kutuma fedha ka matrafiki na familia zao nyumbani walikotoka.
Alisema: Ni fursa na heshima kubwa kushinda tuzo hii. Nilipokuwa nikikuwa nchini Somaliland, niliona jinsi fedha zinazotumwa nyumbani na wahamiaji zinaweza kubadilisha maisha na jamii nzima.
Nilipowasili mjini London kusoma na kuanza kutuma fedha nyumbani , nilikasirishwa na muda na gharama ya kutuma fedha kupitia maajenti.
Hivyobasi alichukulia swala hilo kuwa lengo lake kutafuta njia bora kufanya kazi hiyo kuwa rahisi na kwa muda mfupi.
Ismail Ahmed - Mwanzilishi na Mwenyekiti wa WorldRemit
Jopo lililoongozwa na jaji mstaafu wa mahakama kuu , Dame Linda Dobbs , lilichagua watu hao katika mwaka wake wa 13.
Lengo lao ni kuwatuza wale walio juu katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara , sayansi, teknolojia na burudani. Ni majina 10 pekee yalio juu yalioorodheshwa.
Meghan Markle alichaguliwa katika orodha ya umma, na elimu lakini hakuorodheshwa miongoni mwa watu 10 bora.

Orodha ya watu weusi wenye ushawishi Uingereza:

  1. Ismail Ahmed - Mwanzilishi na Mwenyekiti wa WorldRemit
  2. Pat McGrath, MBE - Msanii wa urembo na mwanzilishi wa Pat McGrath Labs
  3. Michael Sherman - Mkuu wa mikakati na afisa wa mabadiliko BT
  4. Jacky Wright - Afisa mkuu wa Kidijitali Microsoft
  5. Stormzy - Msanii
  6. Edward Enninful, OBE - Muhariri mkuu wa jarida la Uingereza la Vogue
  7. Ebele Okobi - Mkurugenzi wa sera za umma, Afrika, mashariki ya kati na Uturuki
  8. Paulette Rowe - Mkuu wa malipo na huduma za kifedha Facebook
  9. Lynette Yiadom-Boakye - Msanii
  10. Richard Iferenta - Mshirika , KPMG

Friday, October 25, 2019

JE! WAJUA KUWA PANYA HUPUNGUZA MSONGO WA MAWAZO WANAPOENDESHA GARI?


Magari yanaayoendeshwa na panya 'Ratmobile'
Kujifunza kuendesha magari madogo kunawasaidia panya kupunguza msongo wa mawazo, kulingana na wanasayansi.
Watafiti katika chuo kikuu cha Richmond nchini Marekani walilifunza kundi la panya 17 jinsi ya kuendesha magari madogo ya plastiki kabla ya kuwapatia chakula.
Kiongozi wa utafiti huo Daktari Kelly Lambert alisema kwamba panya hao walihisi kupumzika wakati wa mafunzo hayo, matokeo ambayo yanaweza kusaidia katika kufumbua fumbo la tiba za magonjwa ya kiakili isiouzwa dukani.
Panya hao hawakutakiwa kufanyiwa majaribio ya kuendesha magari mwisho wa utafiti huo.

Ni vipi panya hao walijifunza kuendesha magari?

Dkt. Lambert na wenzake waliunda gari dogo la kielektroniki kwa kushikanisha plastiki katika sahani ya alumini ilio na magurudumu.
Ili kuweza kuendesha gari hilo, panya hukalia sahani hiyo ya alumini na kushikilia waya ya shaba . Hapo ndipo gari hilo linapoanza kwenda huku mnyama huyo akielekeza eneo analotaka kusafiri.
Baada ya mafunzo ya miezi kadhaa , panya hao walijifunza jinsi ya kulifanya gari hilo kusonga lakini pia kubadili mwelekeo wake, waliandika watafiti katika jarida la utafiti wa Ubongo.

Je walipata nini?

Baadhi ya panya hao waliokuwa katika utafiti huo walilelewa katika maabara huku wengine wakiishi katika mazingira mazuri - walikuwa na maeneo mengine ya kuishi.
Baada ya majaribio hayo watafiti walikusanya vinyesi vya wanyama hao ili kupima vipimo vya homoni wenye shinikizo mbali na homoni wanaopigana dhidi ya shinikizo hiyo.
Panya wote walikua na viwango vya juu vya homoni wanaopigana na shinikizo ya kiakili, ambayo wanasayansi wanaamini inaweza kuhusisha na kuridhika kujifunza kitu kipya.
Panya katika gari la PlastikiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionPanya hao walidhibiti gari hilo
Dkt Lambert aliambia kitengo cha habari cha AFP kwamba matokeo hayo yanaweza kuwa muhimu kwa utafiti wa siku za usoni kwa lengo la kupata tiba ya matatizo ya kiakili.
''Hakuna tiba ya schizophrenia ama shikizo ya kiakili na tunahitaji kupiga hatua. Nadhani tunahitaji kuangalia wanyama na majukumu tofauti na kuheshimu kwamba tabia inaweza kubadili kemia ya neva''.